Je, David Owuor ni nabii wa ukweli au wa uongo? Sehemu ya Pili (Part 2)
(Sehemu ya Kwanza https://youtu.be/iJLjhQlmMYc.)
David Owuor ni mtu anayedai kuwa nabii wa kipekee. Ana huduma inyoitwa Ministry of Repentance and Holiness, anayoiendesha katika taifa la Kenya. Owuor amepata umaarufu na kuvuma nchini kote kwa kujitambulisha kama Nabii Mkuu Zaidi wa Yehova. Pia, amedai kuwa yeye ndiye nabii wa mwisho atakayetangulia kurudi kwa Bwana Yesu ulimwenguni, na hivyo kanisa linafaa kusikiza ujumbe wake muhimu wa toba na utakatifu. Kama Owuor ndiye nabii wa kipekee wa mwisho, inafaa kanisa limsikize kwa makini. Lakini yafaa tuchunguze madai yake kama ni ya kweli kutoka kwa Biblia. Katika video hii, Joe Thwagi wa ACFAR Kenya, anachunguza zaidi madai ya Owuor na kuyalinganisha na ukweli wa Biblia.